Yakiwa ni maandalizi kuelekea kurejea kwa mikiki mikiki ya ligi kuu ya Vodacom Februari 13, Jumamosi ya Februari 06, kikosi cha Yanga kitashuka kunako uwanja wa Azam Complex, Chamazi kuikabili African Sport ukiwa ni mchezo wa kirafiki
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze atakuwa na nafasi ya kuwapima wachezaji wake kabla ya kuelekea mkoani Mbeya kuifuata Mbeya City ambayo wataanza nayo Februari 13
Aidha akizungumza kwenye tukio la Wananchi Media Day mapema leo, Kaze amesema baadhi ya wachezaji wanarejea taratibu kikosini wakitoka kwenye majeruhi
Saido Ntibazonkiza ameanza mazoezi mepesi wakati Yacouba Songne bado anasumbuliwa na tatizo la misuli
Walinzi Said Juma Makapu na Abdallah Shaibu Ninja ni wagonjwa wakati nyota mpya beki kisiki Dickson Job amepona majeraha na ameanza mazoezi na wachezaji wengine
Kiungo Carlinhos nae yuko fiti akiwa amerejea mazoezini wakati mshambuliaji Fiston Abdul Razak yeye anaendelea kuitafuta 'fitnes'
Kuhusu kiungo Mapinduzi Balama, Kaze amesema nyota huyo anaweza kurejea uwanjani mwezi March