Mambo yote ni Kigamboni leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Feb 2021
Mambo yote ni Kigamboni leo

Siku ya leo ni maalum kwa klabu ya Yanga kujumuika na wadau wake katika tukio lililopewa jina la Wananchi Media Day

Hili ni tukio ambalo litawapa fursa Wanahabari kwa mara ya kwanza kuingia ndani ya kambi ya klabu ya Yanga ilipo ndani ya mji wa kisasa wa Avic Town, Kigamboni

Kupitia tukio hili Wanahabari watapata fursa ya kukutana ana kwa ana na viongozi, benchi la ufundi, wachezaji na wadhamini wa Yanga ambapo watapewa nafasi ya kufahamu masuala mbalimbali yanayoihusu klabu ya Yanga ambayo iko katika sura mpya

Msafara utaanzia Makao Makuu ya Yanga, Jangwani jijini Dar es salaam kuelekea Kigamboni tayari kwa tukio hilo ambalo litaanza saa nne kamili asubuhi

Kila mdau wa Yanga atashiriki katika tukio hilo la aina yake ambalo linafanyika hapa Tanzania kwa mara ya kwanza

Wadhamini wakuu Sportpesa, GSM, Taifa Gas, Afya, Anta na Azam TV wote wamethibitisha watakuwa sehemu ya tukio hilo

Safu ya uongozi wa Yanga itaongozwa na Mwenyekiti Dk Mshindo Msolla, Makamu Mwenyekiti Fredric Mwakalebela, Kaimu Katibu Mkuu Haji Mfikirwa na Arafat Haji, Mjumbe wa kamati ya Utendaji

GSM itawakilishwa na Mkurugenzi wa Uwekezaji Injinia Hersi Said na pia Mshauri wa Yanga Senzo Mbartha nae atakuwa sehemu ya tukio hilo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
1h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
5h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
6h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
9h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’