Afisa Mhamasishaji wa klabu ya Yanga Antonio Nugaz amewaalika Wanahabari, Wanachama,wapenzi na Mashabiki wa Yanga uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere kwa mapokezi ya mshambuliaji Fiston Abdul Razak anayetua leo
Fiston atatua nchini majira ya saa saba na dakika 20 mchana
Ndiye mchezaji pekee ambaye alikuwa akisubirirwa kutua ndani ya kikosi cha Yanga
Umekuwa utamaduni kwa Yanga tangu usajili uliopita, wakiwafanyia mapokezi makubwa wachezaji wa kigeni wanaokuja kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria
Bila shaka leo Wananchi watajitokeza kwa wingi pale JNIA kumkaribisha Fiston
ADVERTISE HERE