Ratiba kombe la FA hadharani, Yanga kushuka dimbani Disemba 24

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2017
Ratiba kombe la FA hadharani, Yanga kushuka dimbani Disemba 24
Michuano ya kombe la FA (ASFC) mzunguuko wa pili itachezwa kuanzia tarehe 20-26 ambapo Yanga inatarajiwa kushuka dimbani Disemba 24, siku moja kabla ya sikukukuu ya XMas kucheza na Reha FC.

Ratiba hiyo iliyotolewa jana inaonesha michezo ya Desemba 20, mwaka itakutanisha timu za JKT Mlale na KMC; Toto African ya Mwanza na Eleven Stars ya Kagera; Ambassador na JKT Oljoro; Boma FC na Ndanda; Mvuvumwa na JKT Ruvu; Abajalo itakuwa mwenyeji wa Tanzania Prisons wakati Milambo ya Tabora itacheza Buseresere ya Geita.

Desemba 21, 2017 Mshikamano itacheza na Polisi Tanzania; Rhino ya Tabora na Alliance ya Mwanza; Majimaji Rangeres ya Lindi itapambana na Mbeya Kwanza ya Mbeya; Njombe Mji na Mji Mkuu ya Dodoma; Ashanti na Friends Rangers za Dar es Salaam; Kagera Sugar na Makambako wakati Stand United ya Shinyanga itacheza na AFC ya Arusha.

Desemba 22, mwaka huu kutakuwa na mechi za Green Warriors na Simba; Polisi Dar itapambana na Mgambo JKT ya Tanga; Kariakoo ya Lindi na Transit Camp ya Dar ila kwa sasa imeweka maskani Shinyanga; Biashara ya Mara itacheza na Mawenzi Market ya Morogoro; Ruvu Shooting ya Mlandizi mkoani Pwani itacheza na Madini FC ya jijini Arusha huku Mufindi United na Pamba ya Mwanza ilihali Singida United itacheza na Bodaboda FC.

Siku ya Desemba 23, mwaka huu Azam FC itacheza na Area C; African Lyon ya Dar es Salaam na Kiluvya United ya Pwani; Makanyagio itapambana na Mbao; Mwadui na Pepsi; Majimaji na New Generation wakati Mbeya City itacheza na Ihefu.

Desemba 24, 2017 Yanga watacheza na Reha FC; Burkina ya Morogoro na Lipuli ya Iringa; Coastal Union ya Tanga na Dodoma Fc ya Dodoma; Shupavu na Real Mojamoja wakati Villa Squad itacheza na Mtibwa Sugar ya Morogoro.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
2h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
17h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
22h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’