Manji aomba afikishwe Mahakamani

Admin By Admin
β€’
5 Jul 2017
Manji aomba afikishwe Mahakamani
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Yanga Yusuf Manji na wenzake wawili wamewasilisha maombi Mahakama Kuu wakiiomba iliamuru Jeshi la Polisi liwafungulie mashtaka mahakamani au liwaachie huru, kulingana na taarifa iliyoripotiwa na gazeti la Mwananchi.

Manji na wenzake Deogratius Kisinda na Thobias Fwere, waliwasilisha maombi hayo mahakamani hapo jana kupitia kwa Wakili Hudson Ndusyepo, baada ya kushikiliwa katika Kituo Kikuu cha Polisi Dar es Salaam, tangu Jumamosi.

Pia, Manji alikumbwa na msukosuko mwingine baada ya watu waliodaiwa kuwa ni wafanyakazi wake kukamatwa na Uhamiaji kwa kuishi nchini kinyume cha sheria wakati si raia na sasa ni hili la kudaiwa kukutwa na nguo za Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Hata hivyo, Wakili Ndusyepo amesema jana kuwa mteja wake huyo yuko Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), anakopatiwa matibabu akiwa chini ya ulinzi.

Jana, wakili huyo alifungua maombi mahakamani hapo dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalumu Dar es Salaam, (ZCO).

Katika hati ya kiapo kinachounga mkono maombi hayo, Wakili Ndusyepo anaeleza kuwa walalamikaji walikamatwa na kushikiliwa na ZCO kwa nyakati tofauti.

Hati hiyo inaeleza kuwa Kisinda alikamatwa Juni 30 saa 10 jioni wakati Manji na Fwere walikamatwa Julai Mosi na saa tano asubuhi, katika jengo la Quality Centre na kwamba wameendelea kushikiliwa Kituo Kikuu cha Polisi hadi sasa.

Katika mahojiano na gazeti la Mwananchi, Naibu Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Lucas Mkondya ameeleza kuwa Manji anashikiliwa tangu Jumamosi ya wiki iliyopita kwa ajili ya mahojiano kuhusu kukutwa majora 43 ya sare za JWTZ na mihuri 39 ya kampuni tofauti na baadhi ya kambi za jeshi.

Ò€œTulipata taarifa kutoka kwa wasiri wetu kwamba katika godauni lililopo katika ofisi zake Chang'ombe anahifadhi sare za JWTZ.

"Tarehe moja mwezi huu tulikwenda kufanya upekuzi wa ghafla ndipo tutakuta majora 35 na kesho yake tukakuta mengine manane na hiyo mihuri,Ò€ amesema Mkondya.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
12h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’