Siku ya leo Alhamisi, Mshambuliaji mpya wa Yanga Fiston Abdul Razak anaweza kutua na moja kwa moja kuelekea kambini kule Kigamboni kuungana wenzake
Jana Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said alisema nyota huyo anatarajiwa kuwasili nchini leo ama kesho akiwa amechelewa kuungana na wenzake kutokana na matatizo ya kifamilia
Yanga ilirejea mazoezini mwanzoni mwa wiki hii kujiandaa na mwendelezo wa ligi kuu na mechi za kombe la FA
Mabingwa hao wa kihistoria wamepania kubaki kileleni mwa msimamo wa ligi mpaka mwezi May watakapokabidhiwa kombe lao
Hii ni ngwe ya lala salama, kocha Cedric Kaze akiwa na matumaini makubwa kwa kikosi chake
Jana benchi lake la ufundi lilikamilika baada ya Nizar Khalfan kutangazwa kuwa kocha msaidizi na Edem Mortotsi raia wa Ghana akitangazwa kuwa kocha wa viungo