Tanzania imeondoshwa kwenye michuano ya CHAN inayoendelea nchini Cameroon baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Guinea katika mchezo wa kukamilisha hatua ya makundi
Tanzania ilihitaji kushinda mchezo huo ili kutinga hatua ya robo fainali na hakika nusura watinge kama sio juhudi zilizofanywa na wachezaji wa Guinea waliofanikiwa kusawazisha bao la pili wakati mchezo ukielekea ukingoni
Baraka Majogoro na Edward Charles Manyama ndio waliokuwa wafungaji wa mabao ya Stars
Wachezaji wa Tanzania walipambana kiume katika mchezo huo kusaka ushindi, bahati haikuwa upande wao
Guinea na Zambia zimefanikiwa kufuzu robo fainali wakati Tanzania na Namibia zinarejea nyumbani
ADVERTISE HERE