Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli afungiwa kujihusisha na soka kwa miaka mitatu baada ya kukaidi hukumu ya Kamati ya Maadili ya TFF ya kulipa faini ya Milioni tano baada ya kupatikana na hatia wakati wa sakata la Bernard Morrison
Dalili za kufungiwa zilionekana mapema baada ya Bumbuli kuitwa na Kamati ya Maadili kwa mara ya pili wakati ambapo alikuwa akisubiri taarifa ya hukumu iliyotolewa awali ili aweze kukata rufaa
Bila shaka Mkuu huyo wa idara ya Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga, anaweza kukata rufaa kupinga adhabu hii
ADVERTISE HERE