Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' usiku wa leo kitashuka dimbani kule Cameroon kukamilisha hatua ya makundi ya michunao ya CHAN kwa mchezo dhidi ya Guinea ambao utapigwa kuanzia saa nne usiku
Tanzania inahitaji kushinda mchezo huu ili kuweza kutinga robo fainali ya michuano hiyo kwa mara ya kwanza katika historia yake
Huu ni mchezo wa kufa na kupona, kocha Etienne Ndayiragije akiahidi vijana wake kuwatoa kimasomaso Watanzania
Mchezo huo utapigwa sambamba na mchezo kati ya Zambia dhidi ya Namibia
Guinea wako kileleni mwa kundi D wakiwa na alama nne sawa na Zambia inayoshika nafasi ya pili
Tanzania iko nafasi ya tatu ikiwa na alama nne, wakati Namibia wao watakamilisha ratiba tu kwa kuwa tayari wameyaaga mashindano hayo wakiwa hawana pointi
Kila la kheri Tanzania...