Mwambusi akerwa na wanaomzushia

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Jan 2021
Mwambusi akerwa na wanaomzushia

Aliyekuwa Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amewataka wanaopotosha kuhusu kuondoka kwake Yanga waache kwani hawamtendei haki

Mwambusi aliuomba uongozi wa Yanga aachie nafasi yake ili aendelee na matibabu ya changamoto za kiafya zinazomkabili

Wiki iliyopita uongozi wa Yanga uliridhia ombi hilo na hivyo kufanya mchakato wa kutafuta kocha msaidizi mwingine

Ni jana tu Nizar Khalfan ametangazwa kuchukua nafasi hiyo iliyoachwa na Mwambusi

Hata hivyo katika mitandao ya kijamii wamejitokeza watu wasio waungwana ambao wanasambaza taarifa za uzushi kuwa kocha huyo ameondoka Yanga kutokana na madai ya mishahara

"Nawaomba wale wanaoeneza habari za uzushi kunihusu mimi na klabu ya Yanga waache mara moja kwani hawanitendei haki mimi wala Yanga"

"Mimi ndiye niliyeandika barua kwa uongozi wa Yanga nikiomba niondoke nikatibiwe baada ya kupewa ushauri na madaktari wangu"

"Sidai chochote Yanga, wala sina tatizo lolote na uongozi wa Yanga. Hii ni mara ya pili nimerudi Yanga hilo linadhihirisha ni kiasi gani Yanga wanatambua, wanajali na kuthamini kile ninachokifanya"

"Nawaomba tuwe na matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii, hakuna haja ya kutumia mitandao kuchonganisha watu na taasisi kwa masuala ambayo hayana ukweli wowote," alisema Mwambusi

Mwambusi anatarajiwa kufanyiwa upasuaji kumaliza changamoto ya jino linalomsababishia maumivu makali ya kichwa

Anatibiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
5h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
17h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’