Ni suala la muda tu Yanga itamtambulisha Nizar Khalfan kuwa Kocha Msaidizi wa mabingwa hao wa kihistoria akichukua nafasi iliyoachwa na Juma Mwambusi aliyeacha majukumu yake kutokana na matatizo ya kiafya
Nizar anatajwa kuwa chaguo la kwanza la kocha Cedric Kaze dhidi ya makocha wengine waliopendekezwa ambao ni Salvatory Edward, Omar Kapilima, Maalim Saleh na Thomas Mourice
Kamati ya Ufundi ya klabu ya Yanga ilikutana mapema leo katika kikao ambacho Kaze alihudhuria
Uongozi wa Yanga ulipendekeza kuteua kocha msaidizi miongoni wa makocha ambao waliwahi kucheza klabu ya Yanga miaka ya nyuma. Huu ni utaratibu ambao hutumiwa na vilabu vingi duniani
Nizar amewahi kucheza Ligi Kuu ya Marekani na akaitumikia Yanga kwa takribani misimu mitatu
Alikuwa mchezaji na baadae Kocha Mkuu wa klabu ya African Lyon