Kazelona imewapa presha huko

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
25 Jan 2021
Kazelona imewapa presha huko

Kasi aliyokuja nayo kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze ni wazi imewapa presha watani zao Simba sasa wanahaha kulisuka upya benchi lao la ufundi

Kaze aliyetua Yanga katikati ya mwezi Oktoba, kwa kiasi kikubwa amefanikiwa kukibadili kikosi cha mabingwa hao wa kihistoria akibaki kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya duru ya kwanza kukamilika

Yanga ya Kaze iko imara sana, ile dhamira ya kutwaa ubingwa msimu huu sasa inaonekana waziwazi

Pamoja na Simba kudai wanafanya usajili kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa, lakini ni wazi kipaumbele chao namba moja ni kukabiliana na Yanga katika mbio za ubingwa wa Bara kwa kuwa huko michuano ya Kimataifa hakuna uhakika wa 'kutoboa' katika kundi walilomo

Simba wameongeza takribani watu wanne katika benchi lao la ufundi akiwemo Kocha Mkuu

Lakini pia wamemsajili mchezaji kama Perfect Chikwende ambaye huyu hawezi kucheza ligi ya mabingwa kwa kuwa tayari ameitumikia Platinum Fc

Pia upo usajili wenye utata ambao unatuhumiwa kufanywa nje ya muda wa usajili, Doxa Gikanji . Inadaiwa Gikanji ameongezwa 'kinyemela' katika kikosi chao kinachocheza ligi kuu wakimuondoa kiungo ambaye walimsajili mapema Taddeo Lwanga ambaye alionekana Zanzibar kwenye michuano ya kombe la Mapinduzi

Aidha Gikanji taarifa zake za usajili Simba zilivuja zikionyesha amesajiliwa akiwa Mtanzania wakati mchezaji huyo yuko Cameroon na kikosi cha DR Congo

Wadadisi wa mambo wanasema huyu anaweza kuwa sababu ya TFF hivi karibuni kutangaza kuongeza muda wa timu kufanya masahihisho ya usajili waliofanya kwenye dirisha dogo kwa wale waliokosea majina ya wachezaji na uraia

Ni wazi ngwe hii ya lala salama ni kufa na kupona kwa Yanga kuhakikisha inatimiza lengo lake la kutwaa ubingwa kwani ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa

Aidha ni wakati ambao TAKUKURU watahitajika sana kutupia jicho nyendo ya baadhi ya timu kwani upo uwezekano wapo watakaofanya hata yasiyowezekana katika mpira ili mradi tu, washinde

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
21m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
46m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’