Kiungo mshambuliaji wa Yanga Farid Mussa usiku wa kuamkia leo aliibuka shujaa wa timu ya Taifa baada ya bao alilofunga kwenye mchezo dhidi ya Namibia kuihakikishia Tanzania ushindi muhimu katika michuano ya CHAN inayoendelea nchini Cameroon
Mussa alichaguliwa kuwa nyota wa mchezo huo uliopigwa huko Limbe, Cameroon kuanzia saa nne usiku
Fundi huyo anayetokea klabu ya Yanga, alikuwa na mchezo mzuri sana, aking'ara eneo la kiungo cha ushambuliaji
Hii ni tuzo kubwa ya kwanza mchezaji wa Tanzania anapata katika michuano hiyo
Kiwango kizuri alichoonyesha kitamuongezea ari na hakuna shaka, ataendeleza moto huo atakaporejea kunako klabu yake ya Yanga
ADVERTISE HERE