Mkongwe Mohammed Hussein ndiye anayeshirikiana na kocha Edna Lema kukinoa kikosi cha Yanga Princess ambacho msimu huu kinawasha moto kwenye ligi kuu ya Wanawake
Yanga Princess imeshinda mechi tisa kati ya 10 walizocheza, sare moja na wanasimama kileleni mwa msimamo wa ligi wakiwa na alama 28
Leo wanakamilisha duru ya kwanza kwa mchezo dhidi ya Allince Girls ambao utapigwa uwanja wa Nyamagana


Mmachinga ameongeza ubunifu kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga Princess wakiwa vinara wa kufunga mabao kwenye ligi
Kwa wasiofahamu, Mmachinga ndiye mfungaji bora wa muda wote ligi kuu ya Tanzania Bara, akiwa amefunga mabao 156
Aidha ni yeye anayeshikilia rekodi ya kufunga mabao mengi ndani ya msimu mmoja, akiweka kambani mabao 26 katika michezo 22 tu
Hii ni rekodi ambayo haijawahi kuvunjwa tangu mwaka 1994