Fiston awakana Mawakala feki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2021
Fiston awakana Mawakala feki

Mapema leo zilisambaa taarifa katika mitandao ya kijamii zinazodai kampuni iliyojitambulisha kumsimamia mchezaji Fiston Abdul Razak imetoa malalamiko kwa TFF wakidai kuwa nyota huyo wa Kimataifa kutoka Burundi amekiuka mkataba baada kujiunga na Yanga bila kuitaarifu kampuni hiyo

Fiston mwenyewe amezisikia taarifa hizo na kueleza kushangazwa na malalamiko hayo huku akisisitiza kuwa watu hao wanaodai kuwa ni Mawakala wake hawafahamu na ni matapeli

"Hao watu waliotoa madai hayo naona ni matapeli, Wakala anayenisimamia mimi niliingia nae mkataba mwaka 2019 naweza kukupatia nakala ya mkataba huo. Lakini pia ndiye niliyeshirikiana nae katika kukamilisha usajili wangu Yanga"

"Wakala huyu nimemalizana nae nimemkabidhi asilimia 10% stahiki yake baada ya kuwa nimesaini Yanga"

"Nina mkataba wa miaka mitatu na Wakala wangu, hivyo taarifa za hao Mawakala wanaojitangaza kwenye mitandao hazina ukweli wowote, " alisema Fiston

Kampuni iliyojitambulisha kwa jina la Heritage agency ilitoa malalamiko hayo kwenda Yanga na TFF wakidai Fiston kakiuka utaratibu wa kimkataba alioingia nao baada ya kusajiliwa na Yanga bila kampuni hiyo kupewa taarifa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
7h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
12h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
16h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
17h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
17h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
Yanga yaondoka Arusha, kituo kinachofuata ni Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’