Kocha Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amejiondoa katika nafasi hiyo kutokana na matatizo ya kiafya
Mwambusi alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu huu akiwa kocha wa muda kabla ya ujio wa Zlatko Krmpotic aliyefanya nae kazi kwa siku 38
Aliendelea kuhudumu katika nafasi ya kocha msadizi hata alipotua kocha Cedric Kaze
Wiki iliyopita alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichoshinda taji la michuano ya kombe la Mapinduzi
Anaondoka Yanga akiiacha timu ikiwa haijafungwa mchezo wowote msimu huu
Kila la kheri Mwalimu Mwambusi..!
ADVERTISE HERE