Hivi yupo wa kushinda dhidi ya hawa jamaa?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2021
Hivi yupo wa kushinda dhidi ya hawa jamaa?

Angalia pale golini wapo kina Metacha Mnata, Farouk Shikhalo na Ramadhani Kabwili, ni msimu ambao Yanga wamepata utulivu sana langoni baada ya kuteseka kwa misimu kadhaa

Wananchi bado wanawakumbuka walinda lango kama Youth Rostand na Clauds Kindoki ambao kuna nyakati walitegemewa!

Mechi 18, cleansheet 11 ni takwimu nadra sana kuzipata kwenye kikosi cha Yanga katika misimu ya nyuma

Sasa angalia safu ya ulinzi, Lamine Moro, Bakari Nondo Mwamnyeto, Abdallah Shaibu, Said Juma, Dickson Job, Kibwana Shomari, Yassin Mustafa, Adeyum Saleh na Paulo Godfrey

Safu ya ulinzi ya Yanga msimu huu imechangia kwa zaidi ya asilimia 70 timu kutopoteza mchezo na kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi

Kuna wakati Yanga ilihitaji ushindi wa bao 1-0 tu kuondoka na alama zote tatu. Lakini kazi kubwa ilifanywa na wababe hawa kuhakikisha lango linabaki salama

Lakini sio kulinda tu hata mabao wanafunga, nahodha Lamine ameweka kambani mabao manne wakati Mwamnyeto amefunga bao moja

Msimu uliopita Yanga iliweka rekodi ya kupata matokeo ya sare nyingi, ni kwa kuwa safu ya ulinzi haikuweza kulinda mabao yaliyokuwa yakifungwa

Kwa wastani, Yanga ilikuwa ikiruhusu bao katika kila mchezo, takwimu ziko tofauti msimu huu

Safu ya kiungo nayo imeimarika. Ujio wa Mukoko Tomombe, Zawadi Mauya wameboresha eneo hilo wakishirikiana vyema na viungo waliokuwepo msimu uliopita Feisal Salum, Deus Kaseke na Haruna Niyonzima

Kocha Cedric Kaze amemfanya Fei Toto kuwa kiungo bora sana msimu huu. Fei Toto ndiye aliyekuwa injini ya timu kabla ya ujio wa Saido Ntibazonkiza ambaye huenda akapewa jukumu hilo na kumuacha Fei Toto abaki na kazi ya kusambaza zile pasi za 'upendo'

Tuisila Kisinda, winga mwenye kasi zaidi kwenye ligi, ameifanya Yanga iwe tishio kwa kila timu inayokuja kucheza nao. Kuna timu zinalazimika kufanya vikao vya dharura kabla ya kucheza na Yanga ili kujua ni jinsi gani wanaweza kumdhibiti 'Tk Master'

Eneo la ushambuliaji lilionekana kuwa na changamoto kidogo lakini Kaze ameongeza mtambo mwingine wa mabao Fiston Abdul Karim katika dirisha dogo la usajili

Ujio wa mwamba huyu utaongeza makali pale mbele na bila shaka atamsaidia Michael Sarpong kuimarika

Ni wazi kwa sasa haitakuwa rahisi kwa Yanga kukubali kupoteza mchezo, ari ya ushindi imetawala kwenye kikosi cha Yanga

Huu unaweza kuwa msimu ambao Yanga inaweza kuweka rekodi nyingine ya kuwa mabingwa bila kupoteza mchezo!

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’