Kaze atamba na kikosi cha kazi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
21 Jan 2021
Kaze atamba na kikosi cha kazi

Baada ya kuongeza nyota watatu dirisha dogo, kocha mkuu wa Yanga Cedric Kaze anaamini kikosi chake sasa kimekamilika na wako tayari kupigania ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom

Yanga ndio vinara wa ligi wakiwa na pointi 44, baada ya kushuka dimbani mara 18, wakiwa mbele ya watani zao Simba kwa tofauti ya alama tisa pamoja na kuwa Simba bado wana michezo mitatu ya kiporo

Kaze mesema ana kikosi imara ambacho kina uwezo wa kupambana na timu zote zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa sababu ndio mashindano makubwa waliyonayo pamoja na michuano ya Kombe la FA.

Kocha huyo alisema alilazimika kuongeza 'majembe' katika kikosi chake kwa sababu anafahamu wazi hakuna mechi nyepesi kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara na Kombe la FA ambayo inachezwa kwa mtindo wa mtoano.

"Malengo yetu msimu huu ni kuchukua ubingwa, ninajua wanachokitaka mashabiki wa Yanga, nimekuja kuwapatia furaha hiyo, malengo yetu ni kuwa na msimu yenye furaha, tumejiandaa na tumejipanga kupambana na timu zote, hatutadharau mchezo wowote," alisema Kaze.

Aliongeza amekuwa akiwapa mbinu tofauti wachezaji wake ili kucheza kwa malengo na kwa sasa kila mmoja anatekeleza maelekezo kwa kiasi kikubwa.

"Wachezaji wangu wanazidi kuwa bora na imara kila siku zinavyokwenda, tunakumbushana mbinu mbalimbali kulingana na aina ya timu tunayokutana nayo, kikubwa ni kuendelea kupambana kuchukua pointi katika kila mechi ili tufikie malengo," Kaze aliongeza.

Kuhusu kiungo nyota wa timu hiyo, Carlos Carlinhos, alisema anatarajia kurejea kikosini kuungana na wachezaji wenzake baada ya majeraha yake kuendelea vizuri.

Alisema kwa sasa kiungo huyo yupo tayari kuanza mazoezi mepesi, ikiwamo ya kwenda Gym, lakini akiendelea kufuata programu nyingine chini ya usimamizi wa madaktari kabla ya kuungana na wenzake atakapokuwa fiti kuanza kuingia uwanjani

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
3h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
19h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’