Kikosi cha Yanga kinajifua kwa nguvu kujiandaa na mzunguuko wa 12 ligi kuu ya Vodacom ambapo mchezo unaofuata ni dhidi ya Mbao FC, Disemba 29.
Kabla ya mchezo huo Yanga itashuka dimbani kati ya Disemba 22-26 kuumana na Reha FC kwenye mchezo wa kombe la FA (ASFC)
Kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina amewaongeza vijana wake kwenye mazoezi maalum ya Gym na mazoezi ya jioni kwenye dimba la Uhuru.

Aidha wachezaji Ibrahim Ajib, Raphael Daudi, Ramadhani Kabwili na Gadiel Michael wanatarajiwa kuungana na wenzao wakati wowote wiki hii baada Kilimanjaro Stars kuondoshwa kwenye michuano ya Chalenji nchini Kenya.
Yanga bado itaendelea kuwakosa wachezaji walio kwenye kikosi cha Zanzibar Heroes ambayo imetinga nusu fainali ya michuano ya Chalenji na itaivaa Uganda Disemba 15.

Kelvin Yondani atakuwa nje kwa muda wa wiki mbili baada ya kuumia nchini Kenya huku Thabani Kamusoko akiwa bado anaendelea na matibabu ya jeraha la goti.

ADVERTISE HERE