Meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema anaamini wataweza kupata matokeo mazuri katika mchezo wao wa kwanza michuano ya CHAN dhidi ya Zambia ambao utapigwa kesho Jumanne
Nadir amesema wamefanya maandalizi kamili ya kutosha na wako tayari kuikabili Zambia
"Tumejipanga na tumejiandaa vizuri, tuko tayari, na sasa ni juu ya kocha wetu kuchagua wachezaji 11 kwa mechi ya kwanza"
"Kocha wetu aliiangalia Zambia dhidi ya Cameroon wakati wa mchezo wa kirafiki na tunaangalia pia video zao ili kuona ni jinsi gani tunaweza kupambana nao
"Tunataka kujua madhaifu yao, Zambia ni timu kubwa yenye wachezaji wazuri. Nakumbuka katika mchezo wangu wa mwisho kwenye mashindano haya mnamo mwaka 2009, tulitolewa na Zambia baada ya sare ya 1-1. Haitakuwa mechi rahisi dhidi yao, lakini tumejiandaa kuanza vizuri kwenye mashindano," alisema Cannavaro
Stars imepangwa kundi D ikiwa pamoja na Zambia, Namibia na Guinea
Baada ya mchezo dhidi ya Zambia, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Namibia kisha kumaliza mechi za makundi kwa kuikabili Guinea
Ratiba ya mechi za wiki hii
