Mwambusi aponda kiwango kibovu Kili Stars

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
•
12 Dec 2017
Mwambusi aponda kiwango kibovu Kili Stars
Kocha wa zamani Yanga Juma Mwambusi ameponda kiwango kibovu kilichoonyeshwa na timu ya Taifa ya Tanzania bara (Kili Stars) kwenye michunao ya Chalenji nchini Kenya.

Kili Stars imeondoshwa kwenye michuano hiyo huku ikiwa imeambulia alama moja pekee kutoka michezo minne.

Mwambusi ambaye amewahi kufanya kazi kama kocha msaidizi wa Yanga ameonesha kusikitishwa na matokeo hayo mabovu na kubainisha kuwa huenda ugeni wa mwalimu ukawa moja ya tatizo kwa timu hiyo kushindwa kufanya vyema.

“Kinachosikitisha watanzania ni timu yetu kufanya vibaya sana katika mashindano ya Chalenji yanayoendelea kule Kenya. Kubwa kama mwalimu ni kuelezana ukweli, watanzania wanataka matokeo mazuri kitu ambacho kocha aliyeteuliwa na wachezaji lazima wajitume na kujitolea kwa ajili ya nchi yao.”

“Timu ya Taifa watu wanaitegemea ni kigezo gani TFF wanakitumia kuteua kocha ni swali ambalo nimekuwa nikiulizwa na wadau wengi wa soka kwa sababu wanaamini kutokana na taaluma yangu na uzoefu huenda nikawa najua, lakini hata mimi sifahamu TFF ndio wenye majibu na wanatakiwa kuwajibu watanzania wapenda michezo kwamba ni vigezo vipi wanavyovitumia.”

“Mwalimu huyu ni mgeni katika soka la Tanzania labda kama alicheza lakini hajafundisha kwa sababu lazima ufundishe vilabu vya ligi kuu ili uweze kuteuliwa mwalimu wa timu ya taifa, lakini sio kufundisha tu umefanya nini katika klabu au vilabu ulivyofundisha. Una wasifu mzuri unawajua watanzania unajua utamaduni wa wachezaji wetu, kwa sababu mwalimu anaweza kuwa mzuri lakini anafundisha katika mazingira yapi na yeye katoka mazingira gani?”

“Watanzania wataendelea kuumia hadi lini kutokana na matokeo ya timu yao ya taifa? Isiwe sehemu ya kujaribia makocha ni kutowapa thamani watanzania ambao mioyo yao inapenda sana matokeo mazuri kutoka kwa timu yetu.”

“Nakumbuka Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassani Mwinyi aliwahi kusema “timu yetu imekuwa kichwa cha mwendawazimu” kwa hiyo kuifuta hii kauli ni lazima tufanye vizuri. Inatakiwa timu iwe na mwelekeo, naishauri TFF kwamba walimu wapo waliofundisha ligi kuu wamefanya vizuri wanatakiwa wapewe nafasi wafundishe timu ya taifa tumechoka kuumia, timu ya taifa sio sehemu ya kwenda kujifunzia au kujaribia.”

“Wachezaji tutawalaumu lakini labda waliletewa utamaduni ambao hawajauzoea na wao wanatakiwa kujituma katika timu yao kwa sababu sisi watanzania tunaumia.”
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE →
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
14h ago
READ MORE →
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE →
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE →
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE →
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE →
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE →