Kaze atamba usajili wa Fiston

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
17 Jan 2021
Kaze atamba usajili wa Fiston

Juzi saa chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa, Yanga ilitambulisha usajili wa mshambuliaji Fiston Abdul Razak, nyota wa Kimataifa wa Burundi

Usajili wa Fiston ulikuwa wa tatu katika kipindi cha dirisha dogo la usajili, Yanga pia ikiwasajili Saido Ntibazonkiza na mlindi Dickson Job

Fiston alisubiriwa sana na mashabiki wa Yanga kutokana na uhitaji wa nafasi anayocheza

Baada ya mwamba huyo kutua, Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema Wananchi watarajie kuona mambo mazuri kwani amemleta mtu ambaye atafanya majukumu mawili kwa ufasaha, kufunga na kutengeneza nafasi za mabao

Aidha Kaze amesema mchezaji huyo atakuja kuongeza chachu katika falsafa yake ya soka anayoijenga kwenye kikosi cha Yanga

"Fiston ni chaguo na mapendekezo yangu, kwa hiyo kuja kwake kumekuja kunogesha falsafa yangu ambayo najaribu kuitengeneza"

"Ni mchezaji anayejua kufunga na kutengeneza nafasi za mabao, namjua vizuri na amekuja kucheza kwenye kikosi cha kwanza, hivyo wapinzani wajiandae tu," alitamba Kaze

Wanayanga watarajie kumuona dimbani karibuni Yanga ikitarajiwa kucheza mechi za kirafiki wakati huu ambao ligi imesimama kupisha michuano ya CHAN iliyoanza jana nchini Cameroon

Michuano hiyo itamalizika Februari 07

 

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11m ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
15h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
20h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
1d ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’