Jumanne, Januari 19 2021 kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kitashuka dimbani huko Cameroon kucheza mechi yake ya kwanza michuano ya CHAN dhidi ya Zambia
Etienne Ndayiragije ambaye ni Mkufunzi wa Stars, amesema wanajipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo wa ufunguzi ili kuwa na nafasi ya kuvuka hatua ya makundi
Stars itahitaji angalau alama nne ambazo zinaweza kupatikana kwa kushinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mwingine ili kuweza kutinga hatua ya mtoano
Mechi nyingine mbili ambazo Stars itacheza hatua ya makundi ni dhidi ya Guinea na Namibia





ADVERTISE HERE