Wananchi kurejea Dar na kombe lao leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Jan 2021
Wananchi kurejea Dar na kombe lao leo

Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea jijini Dar es salaam leo, Ijumaa saa 9:30 Alasiri wakitokea visiwani Zanzibar ambako walitwaa taji la kombe la Mapinduzi

Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amewataka mashabiki kujitokeza kwa wingi Bandarini kuwalaki vijana wao ambao wamewapa heshima katika michuano hiyo kwa kuibuka mabingwa wakiwafunga watani zao Simba kwenye mchezo wa fainali

"Timu itarejea kesho (leo) mchana kutoka Zanzibar. Msafara utajumuisha wachezaji, benchi la ufundi na viongozi wa wachache. Tunawaalika mashabiki wetu waje kwa wingi walipokee kombe lao ambalo wachezaji wetu wameshinda huko Zanzibar," alisema Bumbuli

Yanga ilitwaa michuano ya kombe la Mapinduzi juzi kwa ushindi wa mikwaju ya penati 4-3 dhidi ya watani zao Simba katika mchezo wa fainali ambao dakika 90 zilimalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
13h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
19h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
22h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
23h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
1d ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’