Kilimanjaro Stars imeiaga kwa aibu michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wenyeji Kenya katika mchezo wa mwisho wa kundi A.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na refa Alex Muhabi aliyesaidiwa na Dick Okello na Ronald Katenya, wote wa Uganda, bao pekee la Harambee Stars lilifungwa na Vincent Ouma dakika ya 19, akimalizia mpira uliotemwa na kipa Peter Manyika baada ya krosi ya Ochieng Ovella aliyempita beki Kennedy Wilson.
Stars imeambulia alama moja pekee baada ya kupata sare moja na kupoteza michezo mitatu.
Mapema kabla ya mchezo huo Zanzibar Heroes ambayo tayari ilikuwa imefuzu hatua ya nusu fainali ilichapwa bao 1-0 na Libya.
Zanzibar Heroes itaivaa Uganda kwenye mchezo wa pili wa nusu fainali Disemba 15 wakati wenyeji Kenya wataivaa Burundi Disemba 14 katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali.
Fainali za michuano hiyo zitapigwa Disemba 17

ADVERTISE HERE