Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema vijana wake wako tayari kuelekea mchezo wa fainali michuano ya kombe la Mapinduzi dhidi ya Simba utakaopigwa saa mbili na robo usiku uwanja wa Amaan
Akizungumzia maandalizi ya kikosi chake, Kaze amebainisha kuwa wachezaji wake wako tayari kwa mchezo huo unaosubiriwa kwa hamu na mashabiki wa soka nchini
Aidha Kaze amebainisha kuwa ni mshambuliaji Yacouba Songne mwenye hatihati ya kukosekana leo baada ya kupata majeraha katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Azam Fc
"Ni mechi muhimu ya fainali, tunajua ni mechi ya mwisho, na muhimu zaidi tunacheza na timu nzuri hivyo tunatarajia kuwa na mchezo wenye ushindani. Matumaini yetu ni kuwa baada ya dakika 90 tunatarajiwa kupata matokeo mazuri"
"Wachezaji wote wako katika hali nzuri isipokuwa mshambuliaji Yacouba Songne ambaye alipata majeraha kwenye mchezo uliopita. madaktari wetu bado wanamuangalia kuona kama tunaweza kumtumia katika mchezo huo," alisema Kaze baada ya mazoezi ya mwisho jana jioni