Dabi la Kariakoo linapigwa visiwani Zanzibar ambapo watani wa jadi Yanga na Simba wanachuana katika mchezo wa fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi
Siku zote hakuna mechi ndogo inayozikutanisha Yanga na Simba ndio maana baada ya timu hizo kutinga fainali, habari kubwa iliyozungumzwa zaidi ni mchezo baina yao huko Zanzibar
Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema anawaamini wachezaji wake waliofanikisha timu ikatinga fainali lakini upo uwezekano mwamba Saido Ntibazonkiza akawa sehemu ya kikosi leo
Ntibazonkiza alisafiri na timu visiwani Zanzibar lakini hakushiriki mechi za awali baada ya kuumia
Yeye na Carlinhos waliondolewa kwenye kikosi kutokana na majeraha waliyopata
Lakini sasa mwamba yuko fiti na pengine ikimpendeza kocha Cedric Kaze, anaweza kumjumuisha kwenye kikosi chake leo
Timu zote zitawakosa wachezaji sita kwa kila timu ambao wako timu ya Taifa ambayo Alfajiri ya kesho wataondoka nchini kuelekea Cameroon kushiriki michuano ya CHAN inayoanza Januari 16
Nyota wa Yanga walio timu ya Taifa ni Yassin Mustafa, Bakari Nondo Mwamnyeto, Feisal Salum, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Farid Mussa