Bao la Ayubu Lyanga alilofunga kwenye dakika ya 51 limeinusuru Tanzania na kipigo kutoka kwa DR Congo katika mchezo wa Kimataifa wa kirafiki uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa ambao ulimalizika matokeo ya sare ya bao 1-1
Krosi mahiri ya Ditram Nchimbi ilitendewa haki na Lyanga aliyewazidi ujanja walinzi wa DR Congo pamoja na mlinda lango wao
Ulikuwa mchezo ambao Stars ilipooza kwenye kipindi cha kwanza, wachezaji wakionyesha mabadiliko katika kipindi cha pili
Kocha Etienne Ndayiragije ana kazi ya kufanya kuhakikisha Stars inafanya vizuri katika michuano ya CHAN inayoanza Januari 16 huko Cameroon
Mchezo huo pia ulitumika kumuaga mkongwe Aggrey Morris aliyestaafu kuitumikia timu ya Taifa
ADVERTISE HERE