Kili Stars kukamilisha ratiba dhidi ya Kenya leo

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Dec 2017
Kili Stars kukamilisha ratiba dhidi ya Kenya leo
Hatua ya makundi ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA Chalenji inayoendelea nchini Kenya, inatarajiwa kukamilishwa leo kwa michezo mitatu.

Saa 8:00 mchana, Zanzibar watamenyana na Libya Uwanja wa Jomo Kenyatta, Machakos mchezo ambao utafuatiwa na mechi kati ya wenyeji, Kenya dhidi ya vibonde, Tanzania Bara Saa 10:00 jioni, zote zikiwa mechi za Kundi A, wakati Uwanja wa Kakamega kutakuwa na mchezo mmoja wa Kundi B kati ya Sudan Kusini na Burundi kuanzia Saa 9:00 Alasiri.

Kocha Mkuu wa Kilimanjaro Stars, Ammy Ninje amesema hataki kuondoka Kenya na pointi moja pekee bali angalau washinde na kupata pointi nne.

Amesema wengi wanauchukulia mchezo huo ni kama wa kukamilisha ratiba, lakini kwao wanaingia kwa nia ya kushinda kwa sababu ni mechi ya ushindani na kila anayecheza anahitaji kushinda.

Stars ina alama moja iliyotokana na sare dhidi ya Libya. Ilichapwa michezo yake miwili dhidi ya Zanzibar Heroes ambayo tayari imetinga nusu fainali na mchezo dhidi ya Rwanda.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
2h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
6h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
7h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’