Kikosi cha Yanga kimetinga fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kupata ushindi wa mikwaju ya penati 5-4 dhidi ya Azam Fc baada ya mchezo kumaliza dakika 90 kwa matokeo ya sare ya bao 1-1
Tuisila Kisinda 'TK Master' aliitanguliza Yanga kwa bao safi lakini Azam Fc wakachomoa kupitia kwa Obrey Chirwa
Leo vijana wa Yanga walikuwa taratibu sana dhidi ya Azam Fc lakini muhimu wamepata ushindi uliowapeleka hatua ya fainali
Akizungumza baada ya mchezo huo, Kocha Cedric Kaze amewapongeza vijana wake kwa kufanikiwa kutinga fainali sasa wakiwekeza nguvu zao katika mchezo huo
Kaze amesema leo walipata upinzani mkali kutoka kwa Azam Fc ambao nao wana kikosi imara
Yanga inamsubiri mshindi wa mchezo kati ya Simba dhidi ya Namungo Fc utakaopigwa saa mbili usiku