Jioni ya leo saa 10 Yanga itashuka uwanja wa Amaan visiwani Zanzibar kuikabili Azam Fc katika mchezo wa nusu fainali michuano ya kombe la Mapinduzi
Azam Fc ilitinga nusu fainali kutoka kundi C baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Malindi usiku wa jana
Huu ni mchezo wa kisasi kwa Yanga, mara ya mwisho walipokutana na Azam Fc katika michuano hiyo, walipoteza kwa mabao 3-0
Yanga wakiwa hawajapoteza mchezo wowote katika mechi zote walizocheza mpaka sasa msimu huu, wanatakuwa na mtihani mwingine wa kusaka ushindi dhidi ya Azam Fc ambayo waliichapa bao 1-0 kwenye mchezo wa ligi kuu
Aidha kwa mara ya kwanza kocha wa Azam Fc George Lwandamina anakutana na waajiri wake wa zamani Yanga, hivyo ni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali

Ushindi kwa Yanga utawapeleka fainali na wakati huohuo kama watani zao Simba nao wakishinda mchezo wao wa nusu fainali dhidi ya Namungo Fc, miamba hao wa soka watakutana kwenye fainali