Cedric Kaze, kocha wa viwango vya Kimataifa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Jan 2021
Cedric Kaze, kocha wa viwango vya Kimataifa

Mjumbe wa Kamati ya Utendaji klabu ya Yanga Dominick Albinus amemchambua kocha mkuu wa timu hiyo Cedric Kaze ndiye sababu ya amani na furaha ambayo Wanayanga wanayo leo

Tangu ujio wake Yanga, Kaze amefanikiwa kutengeneza kikosi imara ambacho mpaka sasa hakijapoteza mchezo wowote katika michezo 13 aliyoongoza

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii, Albinus amefunguka mengi kuhusu historia ya kocha Cedric Kaze;

Nimemtazama Kocha Cedric Kaze, nimeitazama tena Yanga ikiwa inacheza kisha nikamtazama tena yeye, nikasafiri mbali sana kupitia makabrasha yake

Bwana Kaze huyu ana leseni A ya CAF na Leseni A ya Chama cha soka Ujerumani (DFB) ndio leseni ngumu zaidi ya ukocha kupatikana duniani, kifupi jina lake lipo kwenye daftari moja na wakina Jurgen Klopp

Kaze huyu ndie alikuwa Mchambuzi wa viwango kwa timu ya Taifa ya Ujerumani chini ya miaka 21, kilichotwaa kombe la dunia 2009, weka nukta hapo

Yaani Ujerumani walimpa majukumu nyeti sana Kaze huyu alipewa kazi maalum na taifa la Ujerumani kufuatilia viwango vya viungo wao ingali wadogo, Toni Kroos, Sami Khedira na Mesuit Ozil, aliifanya kazi na akaikamilisha kazi Kwanini namtaja sana Kaze leo??

Naachaje kumtaa kama mnamwona Kibwana Shomari mchezaji kinda amebadilika kabisa anachukua mali eneo lake, anatunza mali kwa kujiamini na anaitoa kwa kujiamini

Naachaje kumtaja Kaze kama ndie amempeleka Fei Toto mgahawani kisha achague Menu anayotaka, alichofanya yeye ni kumlipia bill yake, akamuweka sawa Mukoko, akawaambia Yanga chezeni kwa kumtazama huyu mtoto, nadhani mnamwona

Naachaje kumtaja Kaze kama sio yeye aliemuibua Saido Ntabazonkiza ingali kinda, akacheza michezo ya Rolling stone pale Arusha, akaenda Ulaya na karudi tena kwenye mikono yake, tukionacho kwake ni matokeo ya akili ya Kaze, aliesema mpeni mpira aamue yeye

Natamani sana nimalize kwa kusema nyuma ya ubora wa Yanga Afrika ni huyu Kaze, natamani tumsake yule Mswahili aliesema 'Ngoja ngoja huumiza matumbo' tumuombe atengue kauli

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
37m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
4h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’