Mshambuliaji wa Yanga Michael Sarpong leo ameongeza mwaka mwingine ikiwa ni kumbukumbu ya siku yake ya kuzaliwa
Mghana huyu ana kitu lakini bado hajaweza kuwaonyesha Wananchi
Sarpong yuko katika presha kubwa, licha ya kuwa ameifungia Yanga mabao manne ndani ya ligi kuu ya Vodacom msimu huu
Amepoteza nafasi kwenye kikosi cha kwanza huku kukiwa na tetesi kuwa anaweza kuuzwa
Kwa mshambuliaji wa aina yake ambaye takwimu zake za mabao katika ligi alizotoka ziko juu, presha anayokutana nayo sasa ilitarajiwa
Anapaswa ni kuhakikisha anaongeza ufanisi langoni kwa kufunga mabao mengi ili kuwanyamazisha wote wanaomkosoa
Huu ni mwaka mwingine kwake, apambane adhihirishe thamani yake
Happy Birthday Sarpong...!
ADVERTISE HERE