Yanga imetinga nusu fainali michuano ya kombe la Mapinduzi wakiwa vinara wa kundi A baada ya kujikusanyia alama nne
Ushindi wa mabao 2-0 waliopata Namungo Fc dhidi ya Jamhuri umeihakikishia Yanga kumaliza vinara kundi A wakifuatiwa na Namungo Fc wenye alama tatu
Baada ya kutumia nguvu kubwa mchezo dhidi ya Yanga, Jamhuri Fc wamejikuta wakifungwa na Namungo Fc 'kiulaini' na kumaliza mkiani mwa kundi A
Namungo wanasubiri kukamilika kwa mechi za makundi kuona kama wana nafasi ya kutinga nusu fainali kupitia 'best looser'
ADVERTISE HERE