Mchezo wa kwanza wa kombe la Mapinduzi kati ya Yanga dhidi ya Jamhuri Fc umemalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana
Ulikuwa mchezo ambao kocha Cedric Kaze alibadili mbinu zake akiwapa nafasi wachezaji wengi ambao hawakupata muda wa kutosha kucheza kikosini
Kaze alifanya mabadiliko kwenye kipindi cha pili, mabadiliko ambayo yaliiongezea kasi Yanga
Hata hivyo safu ya ulinzi ya Jamhuri ilikuwa imara, pongezi nyingi akistahili mlinda lango wa timu hiyo akifanya kazi kubwa ya kuokoa michomo mingo langoni
Yanga itashuka tena dimbani Januari 08 kuikabili Namungo Fc
ADVERTISE HERE