Leo ndio siku ya mwisho kwa Makampuni kuwasilisha makabrasha yao ya zabuni kwa ajili ya ujenzi wa Hostel na viwanja vya mazoezi vya klabu ya Yanga huko Kigamboni
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa Yanga, imebainisha kuwa zoezi hilo lililoanza Novemba 18 2020, litakamilika saa 9:00 Alasiri leo, Makao Makuu ya klabu Mtaa wa Twiga na Jangwani jijini Dar es salaam
Kampuni zote zilizochukua makabrasha ya zabuni, zimeaswa kuhudhuria tukio la ufunguaji wa Tenda ambalo litafanyika Jangwani leo
ADVERTISE HERE