Kikosi cha Yanga kinaelekea visiwani Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi ambapo kesho Jumanne watashuka uwanja wa Amaan kucheza mchezo wao wa kwanza dhidi ya Jamhuri
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema safari hii wamejipanga kurejea jijini Dar es salaam na ubingwa wa michuano hiyo
Yanga inatarajiwa kutumia kikosi chake kamili katika michuano hiyo ili kuwapa raha mashabiki wake visiwani Zanzibar
Ni wachezaji sita tu wanaokabiliwa na majukumu ya timu ya Taifa ndio hawatakuwepo huko visiwani Zanzibar
Aidha kocha Cedric Kaze atatumia michuano hiyo kuendelea kuimarisha kikosi chake kujiweka sawa kukamilisha ngwe ya lala salama ligi itakaporejea baada ya fainali za CHAN
Yanga imepangwa kundi A sambamba na timu za Jamhuri na Namungo Fc
Watacheza na Namungo Januari 08, uwanja wa Amaani
Michezo yote itaanza saa mbili na robo usiku
