Vinara wa ligi kuu ya Vodacom Yanga wana jambo lao kule Rukwa kesho wakitarajiwa kuwakabili Tanzania Prisons katika mchezo wa kufunga mwaka 2020, ligi kuu
Yanga imeondoka mkoani Mbeya kusogea eneo la tukio, uwanja wa Nelson Mandela ndipo mtanange utapigwa hapo kesho
Mabingwa hao wa kihistoria waliweka kambi ya takribani wiki moja mkoani Mbeya kujiwinda na mchezo huo wa kwanza duru ya pili ambao ni mzunguuko wa 18
Afisa Habari wa Yanga Hassan Bumbuli amesema wanakwenda Sumbawanga waifahamu wanakabiliwa na mchezo mgumu dhidi ya Tanzania Prisons inayotumia uwanja wa Nelson Mandela
Hata hivyo amesema anaamini Wananchi wataendeleza moto wao kwenye ligi. Pamoja na kuwa ugenini, lakini ni kama wao ndio wako nyumbani wakitarajia sapoti kubwa ya mashabiki wao hapo Sumbawanga