Katika mechi 13 ambazo Yanga imeshinda msimu huu kwenye ligi huku mlinda lango Metacha Mnata akiwa langoni, michezo 11 hakuruhusu bao
Mechi 16 ameruhusu mabao matano, ameokoa michomo 14 ya hatari na muhimu zaidi aliokoa mkwaju wa penati dakika za majeruhi mchezo dhidi ya Namungo Fc
Metacha amekosa mchezo mmoja tu mzunguuko wa kwanza ligi kuu ya Vodacom

Mjadala umekuwa mkali baada ya mlinda lango huyo kuachwa kwenye kikosi cha Stars kinachokwenda kushiriki michuano ya CHAN baadae mwezi huu nchini Cameroon
Tutaheshimu uamuzi wa kocha Etienne Ndayiragije kutomjumuisha katika kikosi chake, lakini hakuna ubishi ukizungumzia mlinda lango bora katika ligi kuu ya Vodacom mpaka sasa, Metacha Mnata ndiye
ADVERTISE HERE