Nahodha wa Yanga Lamine Moro anamsaka mwandishi wa habari aliyeposti pasi yake ya kusafiria katika ukurasa wa mtandao wa Instagram
Moro amesema anakusudia kumshitaki Mwanahabari huyo (David Kampista) ambaye ni mtangazaji wa vipindi vya michezo EA Radio
"Ndugu Wananchi, kwa yeyote anayemfahamu huyu mtu anijuze nataka kwenda kumshitaki anieleze kwa nini alibandika pasi yangu ya kusafiria kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram," aliandika Lamine kwenye ukurasa wake wa mtandaoni

Tayari Mwanahabari huyo amefuta bandiko aliloweka baada ya Lamine kubainisha kusudio lake la kumshitaki
ADVERTISE HERE