Tarehe kama ya leo miaka kadhaa iliyopita alizaliwa kiungo fundi kipenzi cha Wanajangwani Haruna Niyonzima 'Baba Mzazi'
Niyonzima amejijengea heshima ya kipekee kwenye kikosi cha Yanga akirejea kwa mara ya pili baada ya kuondoka na kuitumikia Simba kwa misimu miwili
Kwa kutambua umuhimu wake kikosini, ni juzijuzi tu Niyonzima aliongezwa mkataba mwingine wa mwaka mmoja kuendelea kuwatumikia Wananchi
Ni mchezaji mwenye uzoefu mkubwa, uwepo wake kikosini unawapa nafasi wachezaji wanaochipukia kujifunza mambo mengi kupitia kwake
Tunamtakia kila la kheri katika siku hii muhimu
Happy Birthday Niyonzima...!
ADVERTISE HERE