Fainali za michuano ya CHAN inayohusisha wachezaji wa ndani inatarajiwa kuanza baadae mwezi huu nchini Cameroon
TFF imeweka hadharani majina ya wachezaji 30 ambao wataingia kambini Januari 01, 2021 kuanza maandalizi ya michuano hiyo
Kwa Yanga waliojumuishwa katika kikosi hicho ni Yassin Mustafa, Bakari Nondo Mwamnyeto, Feisal Salum, Deus Kaseke, Ditram Nchimbi na Farid Mussa
Hata hivyo kukosekana kwa mlinda lango Metacha Mnata na mlinzi wa kulia Kibwana Shomari kumewafanya wadau wengi wa soka nchini washikwe na butwaa

ADVERTISE HERE