Mshambuliaji wa Kimataifa wa Congo Ferebory Dore anatajwa kukaribia kuvaa uzi wa Wananchi, Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM Mhandisi Hersi Said akiwa mbioni kumalizana nae
Dore amewahi kucheza pamoja na Saido Ntibazonkiza ligi kuu ya Ufaransa na kama atatua Yanga basi Saido atakuwa amehusika katika kumshawishi
Inaelezwa nyota huyo atatua jijini Dar es salaam wakati wowote kukamilisha mazungumzo na uongozi wa Yanga
Hivi karibuni Injinia Hersi alisema kuwa wako mbioni kukamilisha usajili wa mchezaji mahiri mwenye 'cv' kubwa ambaye anakuja kuingia moja kwa moja kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga
Kama ilivyo kwa Ntibazonkiza, Dore (31) amecheza barani Ulaya kwa zaidi ya miaka 10 pia akicheza michezo 37 na kufunga mabao 10 katika timu ya Taifa ya Congo (Brazzaville)
Yanga inatarajiwa kuimarisha safu yake ya ushambuliaji ambapo katika kipindi hiki cha dirisha dogo, imehusishwa na wachezaji watatu wa Kimataifa
Jacquise Tuyisenge (APR) na Idris Mbombo (Nkana Fc) pia walitajwa kuwa katika orodha ambayo Injinia Hersi anayo
Kule nchini Zambia baadhi ya magazeti yameripoti kuwa Mbombo amefichua mpango wake kuondoka Nkana Fc inayokabiliwa na changamoto za kiuchumi ikishindwa kulipa mishahara kwa wakati
Kitendawili cha nani anakuja kuongeza nguvu pale kwenye safu ya ushambuliaji Yanga huenda kitatenguliwa kabla ya mwaka 2020 kumalizika...!