Kocha Mkuu wa Yanga Cedric Kaze amesema kikosi chake kinajiandaa vyema kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Tanzania Prisons ambao utapigwa mkoani Rukwa keshokutwa Disemba 31
Akizugumza baada ya program ya mazoezi jana jioni, Kaze amesema wachezaji wanne wamekosekana mazoezini kutokana na sababu mbalimbali
"Tunaendelea na mazoezi kuwa tayari kucheza na Prisons. Tunafahamu tunakabiliwa na mchezo mgumu kwani Prisons ni timu nzuri. Ni timu chache ambazo zimeweza kupata matokeo katika uwanja wao"
"Wachezaji wangu wako na hali nzuri isipokuwa wachezaji wanne ambao hawako mazoezini kutokana na sababu mbalimbali"
"Ditram Nchimbi tulimruhusu aende akashughulike matatizo ya kifamilia, wakati Ramadhani Kabwili ni majeruhi kama ilivyo kwa Yacouba Sogne na Saido Ntibazonkiza ambao waliumia kwenye mchezo dhidi ya Ihefu Fc"
"Saido na Yacouba tutawaangalia hali zao kwenye mazoezi ya mwisho tuone kama tutaweza kuwatumia Alhamisi," alisema Kaze
Yanga imeweka kambi mkoani Mbeya kukamilisha maandalizi yake kabla ya kuelekea mkoani Rukwa tayari kwa mchezo huo