Beki wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ Kelvin Yondani ataukosa mchezo dhidi ya Rwanda utakaofanyika kesho Jumamosi Desemba 9, 2017 kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos Kenya.
Yondani atakuwa nje kwa wiki mbili baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo wa jana dhidi ya Zanzibar.
Leo kikosi cha Kilimanjaro Stars kimefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Machakos Academy licha ya mvua zinazoendelea kunyesha Kenya.
Kilimanjaro inajiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Rwanda utakaochezwa saa 8 mchana kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos.
Mchezo huo wa kundi A una umuhimu mkubwa kwa Kilimanjaro Stars katika harakati zake za kuitafuta tiketi ya kucheza hatua ya nusu fainali.
Kilimanjaro Stars ina pointi moja mpaka sasa baada ya kutoka sare na Libya kwenye mchezo wa kwanza kabla ya kufungwa na Zanzibar kwenye mchezo wake wa pili.
Kundi A linaongozwa na Zanzibar wenye pointi sita (6) wakifuatiwa na Kenya wenye pointi (4) wakati Libya yenyewe ina pointi (3) ikikamata nafasi ya tatu ikifuatiwa na Kilimanjaro Stars na Rwanda wenye pointi (1) kila mmoja.

ADVERTISE HERE