Duru ya pili tutakuwa bora zaidi - Dk Msolla

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2020
Duru ya pili tutakuwa bora zaidi - Dk Msolla

Mwenyekiti wa Yanga Dkt. Mshindo Msolla ameeleza kuridhishwa na matokeo ambayo Yanga wamepata katika michezo 17 ya duru ya kwanza ya ligi na kuwa na matumaini ya kufanya vizuri katika michezo ya duru ya pili ya kumalizia ligi

Dk Msolla amesema Kocha Cedric Kaze amefanya kazi kubwa ya kutengeneza kikosi imara licha ya kuwa hakuanza na timu tangu mwanzo wa msimu

"Nikizungumza kwa uelewa wangu kama kocha wa soka,inawezekana tukafanya vizuri zaidi katika mzunguko wa pili kwani katika duru hili la kwanza kocha wetu (Cedric Kaze) aliukuta katikati lakini amepambana kuingiza ubora na sasa tuko hivi"

"Kocha amewafahamu wachezaji wake nao wamemjua kocha wao na wanatambua nini anakitaka kutoka kwao

"Baada ya mapumziko ya CHAN na Mapinduzi Cup baada ya kumaliza mchezo wa Prisons, nadhani tutakuwa na timu bora na ngumu zaidi"

"Kama uongozi tunaridhika sana na kazi inayofanywa na makocha wetu kuanzia mkuu wao Kaze lakini pia ubora mkubwa wanaouonyesha wachezaji wetu katika mechi zote 17 walizocheza mpaka sasa," alisema Dk Msolla

Baada ya mchezo dhidi ya Tanzania Prisons, Disemba 31, Yanga itaelekea Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi na baadae kufuata mapumziko ya michuano ya CHAN

Yanga iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikijikusanyia alama 43, wakimaliza duru ya kwanza bila kupoteza mchezo

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’