Bado wanasajili kupitia kivuli cha Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2020
Bado wanasajili kupitia kivuli cha Yanga

Msimu miwili nyuma, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa 'Master' sasa kocha wa Ruvu Shooting, alikuja na mbinu ya usajili wa 'kimyakimya' baada ya kubaini baadhi timu hasa Simba na Azam Fc zilikuwa zikifanya usajili wao kwa kutumia tetesi za usajili wa Yanga

Timu hizo zilisubiri kusikia Yanga wanamtaka nani kisha haraka zinakwenda kusajili, bahati mbaya wakati huo Yanga haikuwa na uwezo mkubwa wa kifedha

Jambo hilo halijabadilika kwani miamba hao wa soka katika sajili zao bado wanapita mulemule kwenye kivuli cha Yanga ingawa usajili uliopita wamelishwa sana 'matango pori'

Angalia baadhi ya wachezaji waliosajiliwa na Azam Fc kama Ally Niyonzima, Awesu Awesu na sasa Mpiana Monzinzi wote walianza kutajwa kuwaniwa na Yanga

Monzinzi alitajwa sana kukaribia kutua Yanga kabla ya mabingwa hao wa kihistoria kumsajili Michael Sarpong aliyekuwa akiitumia Rayon Sports

Hata Simba wachezaji kama Luis Miquissone, Larry Bwalya na hata Ibrahim Ame walitajwa kuwaniwa na Yanga

Zaidi Simba walikwenda mbali zaidi kwa kumsajili Bernard Morrison katika mazingira ambayo yalijaa utata mwingi

Lakini pia katika kikosi cha Simba wapo wachezaji kama Beno Kakolanya, Ibrahim Ajib na Gadiel Michael nao waliwasajili baada ya kumaliza mikataba Yanga

Taratibu mambo yameanza kubadilika kwani tangu ujio wa GSM, Yanga imeongeza umakini katika usajili wake, wameweza kuwasajili wachezaji wote waliowahitaji, katika baadhi ya sajili 'fedhwa' iliongea

Haikuwa kazi rahisi kuunda kikosi imara cha Yanga ambacho kimemaliza duru ya kwanza ligi kuu ya Vodacom bila ya kupoteza mchezo

Injinia Hersi Said upande wa GSM akishirikiana na viongozi wa Yanga, wamefanikiwa kuirejesha heshima ya Yanga kuanzia kwenye usajili

Sasa sio rahisi tena kwa mchezaji anayetakiwa na Yanga kusajiliwa na Simba au Azam

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
2h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
2h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
10h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
14h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’