Kinachopiganiwa na Yanga sio Morrison, ni haki

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Dec 2020
Kinachopiganiwa na Yanga sio Morrison, ni haki

Mwanzoni ilionekana kama utani vile pale uongozi wa Yanga ulipotangaza kulipeleka shauri la Bernard Morrison Mahakama ya Kimataifa ya usuluhishi wa Michezo (CAS)

Wapo walioamini shauri hilo haliwezi kusikilizwa karibuni, lakini taarifa iliyotolewa juzi na Makamu Mwenyekiti wa Yanga fredrick Mwakalebela imetoa mwanga kuwa Yanga inaweza kupata haki yake huko

Kitendo ya utetezi wa Morrison kukataliwa na kesi hiyo kupangiwa Jaji na tarehe ya kuanza kusikilizwa ni ishara kuwa mapema tu, CAS wamebaini kuna mambo hayako sawa

Yanga italipia takribani Milioni 30 ili kesi hiyo iweze kusikilizwa

Morrison wa nini Yanga?

Wapo wanaojiuliza kwa uimara wa kikosi cha Yanga sasa kwa nini bado wanahangaika na Mghana huyo ambaye hata huko alikosajiliwa hana nafasi ya kucheza?

Uongozi wa Yanga kupitia Makamu Mwenyekiti wake, Fredrick Mwakalebela uliweka bayana hili mapema tu kuwa wanaamini hukumu iliyotolewa kubatilisha mkataba ambao Morrison alisaini Yanga haikuwa sahihi

Hivyo wanachokitafuta sasa ni haki ambayo wanaamini wataipata huko katika vyombo vya Kimataifa

Yanga haijali kesi hiyo itachukua muda gani lakini jambo la muhimu kwao ni kuipigania haki ambayo walinyimwa hapa nyumbani

Yanga inataka mkataba uliobatilishwa utambulike kuwa ulikuwa halali, baadae Morrison na klabu ya Simba watalipa gharama ya kile walichokifanya

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
2h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
6h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
11h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
11h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
21h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’