Jana klabu ya Chppa United inayoshiriki ligi kuu ya Afrika Kusini ilimtangaza Luc Eymael kocha wa zamani wa klabu ya Yanga, kuwa kocha mkuu wa timu hiyo
Hata hivyo muda mchache baada ya Chippa United kumtangaza kocha huyo, Chama cha Sokoa Afrika Kusini, kimeiandikia barua Serikali ya Afrika Kusini kupinga Mbelgiji huyo kupewa kibali cha kufanya kazi
Ni kutokana na matamshi ya kibaguzi aliyotoa dhidi ya mashabiki wa Yanga mwishoni mwa msimu uliopita baada ya mchezo dhidi ya Lipuli Fc
Baada ya Yanga kumtimua na TFF kupeleka malalamiko FIFA kutokana na matamshi yake, SAFA ilitangaza kuwa haitamruhusu kocha huyo aliyefanya kazi hapo Afrika Kusini kwa muda mrefu kurejea
Wamesimamia kile walichoahidi, ubaguzi wa rangi hauna nafasi kwenye soka
ADVERTISE HERE