Yanga imefuzu raundi ya nne ya michuano ya kombe la Shirikisho (ASFC) baada ya Singida United kuondolewa kwenye mashindano hayo
Mchezo kati ya Yanga dhidi ya Singida United ulikuwa upigwe Jumamosi Disemba 26 lakini TFF wameiondoa Singida United baada ya kukosa sifa
Singida United imekuwa na ushiriki wa kusuasua ligi daraja la kwanza ambapo timu hiyo imeshindwa kutokea uwanjani katika michezo miwili
Taarifa zaidi kutoka TFF zimebainisha kuwa Singida United imeshushwa madaraja mawili
ADVERTISE HERE